Monday, 27 January 2014

MICHUANO YA KOMBE LA FA YAINGIA RAUNDI YA TANO, CHELSEA NA MAN CITY USO KWA USO


Michuano ya kombe la FA imeingia raundi ya tano ambapo mechi zote zitachezwa Jumamosi na Jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi pili huku Chelsea na Manchester City zikitazamiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Chelsea walifuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila. Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii alisema: Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora.”
Pia Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2
Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano,huku Roberto Martinez akiiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi iliyokutanisha timu zote za ligi ya England.
Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton. Sheffield watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.
Mshindi wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainali yake itachezwa kwenye uwanja wa Wembley.

Source:BBC

PHOTOS: DIAMOND AMNUNULIA WEMA SEPETU ZAWADI NCHINI KENYA.




Diamond Platinumz ambaye alikuwa na music show nchini Kenya juzi aliamua kumnunulia mpenzi wake Wema Sepetu zawadi za perfume na mazagazaga mengine ya urembo ikiwa ni ishara ya wapendanao. kupitia Instagram Wema aliandika....

Angalia picha hapo chini Diamond akimnunulia Wema zawadi huko Kenya........




 

HUYU NDIO MTOTO MZURI NAIMA SHAA MPENZI MPYA WA CLEMENT NI WA YULE KIGOGO WA IKULU ALIYEKUWA MPENZI WA WEMA SEPETU ALIYEMNG'ANYA VITU VYAKE BAADA YA KURUDIANA NA DIAMOND


NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.
 http://baabkubwamagazine.com/wp-content/uploads/2014/01/Naima3_8.jpg
 

Naima Shaa.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).

“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.

Wema Sepetu.



NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.

“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.

“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.

“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.

WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.


Tatoo ya Clement mgongoni mwa Naima.

“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.

UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.

Alipoulizwa kuhusu tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).

“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.

WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.

Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.

“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.

NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.

“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.

“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu.

MAPRO AZAM WABANANA KATIKA CHUMBA KIMOJA



AZAM FC ina utaratibu wa kuwaweka wachezaji wawili wawili katika vyumba vya kambi yake iliyopo Chamazi Mbagala jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo hali ni tofauti kwa wachezaji Kone Muhamad, Balou na Kipre Tchetche ambao wanaishi chumba kimoja kutokana na tatizo la lugha.
Kocha wa Azam, Joseph Omog amependekeza timu yake iweke kambi Azam Complex, katika eneo ambalo uwanja wa mazoezi upo mita chache kutoka vilipo vyumba vya wachezaji.
Kone, Balou na Tchetche wenyewe wanaishi chumba kimoja kwa kuwa wote wanazungumza Kifaransa kwa kuwa kwao Ivory Coast ndiyo lugha ya taifa.
Awali chumba hicho kilikuwa kinatumiwa na pacha Balou na Tchetche ambao wanamudu pia kuzungumza Kingereza, lakini aliposajiliwa Kone, Novemba mwaka jana wanalazimika kuishi naye chumbani humo.
“Kone hawezi kuzungumza lugha nyingine zaidi ya Kifaransa, anashindwa kuwasiliana na wachezaji wengine katika mazingira ya nje ya uwanja. Tupo naye hapa chumbani ili angalau tumfundishe Kingereza ili akimudu naye aweze kuishi na wachezaji wengine,” Tchetche aliliambia Mwanaspoti chumbani humo.
Akizungumza na Mwanaspoti kwa msaada wa Tchetche, Kone alisema anafurahia maisha ya Tanzania, lakini changamoto ya lugha inampa wakati mgumu.
“Nazungumza Kifaransa tu, na ninaoweza kuzungumza nao hapa ni Balou na Tchetche labda na kocha, lakini wachezaji wengine ni tatizo, nikiweza kuzungumza Kingereza nitaenda chumba kingine,” alisema Kone.
Akizungumzia hali hiyo, meneja wa Azam, Jemedari Said alisema wamemkubali Kone kuishi chumba kimoja na raia wenzake wa Ivory Coast ili kupata muda wa kujua Kingereza ili aweze kujichanganya wachezaji wengine.
“Hata Tchetche alipofika hapa alikuwa anakaa na Ibrahim Shikanda, alipojua Kingereza akajichanganya na wengine. Alipokuja Balou akaishi na Tchetche na hadi sasa wapo pamoja,” alisema Jemedari.
CHANZO MWANASPOTI

YALIYOJIRI KWENYE OPERESHENI PAMOJA DAIMA NGARA NA BUKOBA MJINI


NGARA
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa Ngara katika mkutano mkubwa wa Operesheni Pamoja Daima
Mamia ya wakazi wa Ngara waliojitokeza katika mkutano wa Operesheni Pamoja Daima uliohutubiwa na Mh Freeman Mbowe.


BUKOBA MJINI
 Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe(kulia) pamoja na Mh John Mnyika
 Mh John Mnyika akihutubia wakazi wa Bukoba Mjini katika mkutano mkubwa wa Operesheni Pamoja Daima

Umati mkubwa wa watu waliofika kwenye mkutano huo

WEZI WAIBA MILANGO, TAA ZA GARI NA KUWAPORA WAPITA NJIA BAADA YA KUTOKEA AJALI ENEO LA TANDALE JIJINI DAR


 Nissan Patrol namba T479 BPJ baada ya kuigonga Bodaboda eneo la Tandale kwa Bonge, Dar jana usiku.
 WEZI walipora milango, taa za gari na kuwapora wapita njia kufuatia ajali iliyotokea Tandale kwa Bonge jijini Dar es Salaam baada ya gari aina ya Nissan Patrol namba T479 BPJ kugongana na mwendesha Bodaboda ambayo haikujulikana namba zake jana usiku (Jumamosi).
 Dereva na mmiliki wa gari hilo, Alex Mutabazi akiwa amejeruhiwa baada ya kipigo kutoka kwa vibaka.
 Katika vurumai hiyo ambayo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari, vijana wa eneo hilo  walitumia fursa hiyo kung’oa milango na taa za gari hilo na vingine vilivyokuwemo ndani yake na baadaye waliendelea kuwapora wapita njia na watu waliokuwa kwenye daladala zilizokuwa zikipita hapo.

 
  Gari hilo mali ya Alex Mutabazi (59) likiwa limevunjwa kioo cha mbele na vibaka wa Tandale kwa Bonge.
 Dereva na mmiliki wa gari hilo, Alex Mutabazi (59) naye alichezea kichapo kikali kutoka kwa vijana hao. Polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuwatia mbaroni vijana kadhaa waliohusika na uporaji huo.
 Hata vitu vilivyokuwa ndani ya gari hilo pia viliibiwa
 Gari hilo likiwa limeondolewa mlango wa nyuma na vibaka
Vioo vya gari hilo vikiwa vimevunjwa.

MAHAKAMA NKASI YAMUAMURU MUME KUJENGA NYUMBA YA MTALAKA WAKE.


Maria Tarafa (wa kwanza kushoto) akiwa na watoto wake wanne aliozaa na Ndebile Kazuri akiwa sehemu ya nyumba anayokaa, mumewe ameibomoa nyumba hiyo ili kumfukuza eneo hilo.
 
MAHAKAMA ya mwanzo Mjini Namanyere, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imetoa amri ya kumtaka Ndebile Kazuri kujenga nyumba ya aliyekuwa mke wake Maria Tarafa iliyopo kijijini Isale ambayo aliibomoa akishinikiza mtalaka wake aondoke eneo ambalo alikuwa akikaa kabla ya kutengana.

Mwishoni mwa mwaka jana (2013) Mahakama hiyo ilivunja ndoa ya wanandoa hao wenye watoto wanne baada ya Kazuri kuwasilisha kesi mahakamani akitaka ndoa yake na mkewe ivunjwe. Hata hivyo baada ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo mke amewasilisha kesi mahakamani hapo akitaka mali za ndoa hiyo zigawanywe na mume awajibike kuwatunza watoto wake, jambo ambalo halikuzungumziwa kwenye kesi ya awali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, Bi. Tarafa alisema Mahakama ya mwazo imetoa amri ya kumtaka mtalaka wake kujenga nyumba aliyomvunjia yeye na watoto wake wanne akishinikiza aondoke nyumbani hapo, bila kupewa haki ya mgao wa mali zilizochumwa wakati wa ndoa.
 


“…Juzi tumetoka Mahakamani nilikwenda kufungua kesi nikiiomba mahakama igawe mali ambazo tulichuma na mume wangu muda wote wa ndoa yetu lakini mume wangu hataki zigawanywe, ila mahakama imemuamuru kwanza ajenge nyumba ambayo amenivunjia pale nyumbani nikiwa na watoto akitaka niondoke nyumbani, ameambiwa awe ameimaliza kabla ya Februari 14,” alisema Bi. Tarafa akizungumza kwa njia ya simu.

Alisema Kazuri alivunja nyumba ambayo mkewe alikuwa akiishi na watoto wake wanne siku chache baada ya mahakama ya mwanzo wilayani Nkasi kuvunja ndoa yao, jambo ambalo Bi. Tarafa hakukubaliana nalo kwani alitegemea watagawana mali ya ndoa yao na yeye kupata nyumba ya kuishi.

“…Katika muda wote wa ndoa yetu tumefanikiwa kupata mali kama nyumba tatu ambazo zote zipo eneo moja la kijiji cha Isale, ng’ombe zaidi ya 127, mbuzi 30 pamoja na mashamba zaidi ya hekari 70 mali ambazo hazikuzungumziwa kabisa na mahakama, lakini baada ya ndoa kuvunjwa nashangaa mwenzangu ananibomolea hata nyumba ambayo nilikuwa naishi mimi na wanangu…sasa naomba kila mmoja agawiwe haki yake,” alisema Bi. Tarafa.
Kazuri alifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo, Namanyere Wilaya ya Nkasi Oktoba 28, 2013, kesi namba 26/2013 iliyosikilizwa na Hakimu aliyetajwa kwa jina la B. Stanley; na Novemba 18, 2013 hakimu huyo baada ya kuisikiliza kesi aliamuru ndoa ivunjwe.

Mahakama ilivunja ndoa hiyo na kuamuru Bi. Tarafa aondoke na watoto wawili kati ya wanne waliozaa na mumewe kipindi wakiishi kama mke na mume bila kueleza namna watoto hao watakavyo pata huduma toka kwa baba yao.
Mahakama pia iliamuru watoto wa miaka 7 na 9 watabaki kwa baba yao na wenye miaka chini ya saba kubaki na mama yao. Mahakama hiyo ya mwanzo pia iliamuru mke apewe magunia 9 ya mahindi kati ya 10 ambayo walizalisha wote na bati 7 zilizokuwa nyumbani.

Kwa upande wake Kazuri akizungumzia juu ya mali ambazo mkewe anazilalamikia, alisema mali hizo alipewa na babayake wakati anaanza maisha hivyo bado ni mali ya babayake mzazi ambaye alidai yupo hai hadi sasa. Hata hivyo tarifa zaidi zinasema baba yake na Kazuri (Kazuri Moshi) alifariki mwezi Machi 2004 na mali zake kurithishwa kwa watoto wake akiwemo Kazuri.

Katika mgao huo mtalaka wa Kazuri alisema walipewa jumla ya ng’ombe 65 lakini wamezizalisha hadi kufikia idadi kubwa hivi sasa, ambapo ni zaidi ya ng’ombe 127 pamoja na mashamba.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TAMWA

MKUU WA POLISI WILAYA (OCD) IRINGA APATA AJALI


Askari wakitazama gari ambalo alikuwa akiendesha OCD Iringa alililopata ajali nalo majira ya saa 10 jioni jumapili walilikuwa wakielekea katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM kata ya Nduli Iringa mjini hakuna aliyepoteza maisha ktk ajali hii iliyotokea kona la Mgongo barabara ya Iringa-Dodoma
Wasomi wa chuo kikuu cha Iringa wakitazama ajali hiyo ambayo dereva wake OCD Iringa alinusurika kifo na kuumia mkono wake.

Sunday, 26 January 2014

PROFESA MWESIGA BAREGU AFICHUA SIRI YA KUTWANGANA NGUMI NA KUSALITIANA NDANI YA CHADEMA




MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu, amefichua siri ya madai ya usaliti ndani ya chama hicho.

Akizungumza na Mtanzania katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Profesa Baregu alisema kiini cha tuhuma na madai ya usaliti ndani ya Chadema ni kutoaminiana na kukosekana kwa uvumilivu. 

Alisema kitendo cha wanachama na viongozi kunyoosheana vidole vya usaliti kinakiangusha chama na kwamba Chadema kimefeli katika mambo matatu, ambayo ndiyo yanapaswa kuwa msingi wa chama na  kama yangezingatiwa mapema, hoja ya usaliti isingezungumzwa leo.

Aliyataja mambo hayo yanayozalisha hoja nzito ya usaliti iliyosababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho kuvuliwa uanachama kuwa ni kusikilizana, kuvumiliana na kuaminiana.
 

“Kukosekana kwa mambo hayo ndio kiini cha kuibuka kwa hoja ya usaliti, hatua hii ni mbaya katika maendeleo ya chama kinachojijengea uaminifu kwa wananchi,” alisema.

Alisema kuendelea kwa hali ya kushutumiana ndani ya chama kunasaidia kukitafuna na ipo siku Chadema haitakuwa na mtu msafi, kwani wote wataitana wasaliti.

“Chadema ni chama kizuri cha siasa, lakini kimefeli kabisa katika kuyadhibiti mambo hayo matatu muhimu, nadhani hili ni tatizo kubwa linalokiandama chama hiki.

“Matokeo ya hali hii ndiyo yanayozalisha mivutano isiyokuwa na tija, huyu kasema hivi yule naye anasema vile, hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake na kibaya zaidi watu ndani ya chama hawaaminiani, utasikia leo huyu katajwa msaliti, kesho yule, utafika wakati chama hakitakuwa na msafi, wanachama wote watakuwa wasaliti,” alisema Profesa Baregu.

Akizungumzia mgogoro wa hivi karibuni ndani ya chama hicho uliosababisha Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo kuvuliwa uanachama, huku Zitto Kabwe akikimbilia mahakamani, Profesa Baregu alisema hayo ni madhara ya kutotumia hekima na kukosekana kwa busara ya kumaliza tofauti kwa mazungumzo.

“Kama hamsikilizani wala kuaminiana, lazima athari ziwepo, tena kubwa tu, kwa sababu matukio ya namna hiyo yanakuwa endelevu, leo kashutumiwa huyu ni msaliti, huwezi kujua mwingine atashutumiwa lini …na mvurugano uliotokea hivi karibuni  ndio uhalisia  wa kile nilichokisema hapo awali, kwamba ndani ya Chadema kumekosekana utamaduni wa kumaliza tofauti kwa mazungumzo, kwa ujumla watu hawavumiliani wala kusikilizana,” alisema Profesa Baregu.

Aidha alitahadharisha kwa kusema, usaliti utakidhoofisha chama kwa kiasi kikubwa, ambapo  alikitolea mfano Chama cha NCCR-Mageuzi, ambacho kilikumbwa na mazingira kama hayo na mwisho wake kikaparaganyika ovyo kwa sababu kila mtu alijikuta anatazamwa kuwa msaliti.

Wakati huo huo, imebainika kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini haijatoa mwongozo wowote juu ya barua iliyoandikiwa na Mwigamba, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha.  Mwigamba aliitaka ofisi hiyo iingilie kati suala la kunyofolewa kinyemela kwa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama hicho.

Inaelezwa kuwa Mwigamba alifikia hatua ya kuandika barua hiyo kabla hajavuliwa uanachama, ambapo alifanya hivyo baada ya kutokea sintofahamu baina ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto,  Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na wafuasi wanaomuunga mkono Mbowe.

Akithibitisha madai hayo, Mwigamba alisema ni kweli kuwa alimwandikia barua Msajili, ambayo ilikuwa ikihoji ukiukwaji wa katiba ya chama pamoja na kuondolewa kwa kipingele cha ukomo wa muda wa uongozi, hata hivyo mpaka sasa hajapatiwa majibu.

Alisema mara baada ya kuandika barua hiyo, Msajili aliwaandikia Chadema ili kupata ufafanuzi wa madai hayo, ambapo walijibu kuwa walisambaza waraka kwa makatibu wa chama hicho wa mikoa ili kupata uungwaji mkono kabla ya kukiondoa.

Hata hivyo, Mwigamba alilalamikia hatua hiyo kwa madai kuwa inakiuka katiba na utaratibu wa chama hicho na kwamba barua iliyosainiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Shaibu Akwilombe, Julai 13,  2006, kwenda kwa makatibu hao ilikuwa ikiwaarifu kuwa yanapelekwa mapendekezo ya ziada.

Kwamba waunge mkono pendekezo kuwa Katibu Mkuu na manaibu wawili wateuliwe na Mwenyekiti, wasipigiwe kura na majina yao yapelekwe Baraza Kuu kwa ajili ya kupiga kura kuchagua mmoja.

“Katiba ya mwaka 2006 isomeke pia kiongozi anaweza kuchaguliwa tena na ndiyo walileta mapendekezo na mwanzo mpaka mwisho wa barua ilikuwa inaongelea mapendekezo tu. Msajili alinitumia nakala ya majibu yao ili nitoe maelezo ya ziada, ambayo pia nilishafanya hivyo tangu Desemba 30 mwaka jana,” alisema Mwigamba.

Alisema kuwa katika majibu ya Chadema ya Desemba mwaka jana kwa Msajili, yalionesha wazi kwamba Mwigamba alishavuliwa uanachama wa chama hicho, wakati alikuwa bado hajafukuzwa, ambapo walidai kwamba kipengele hicho kilifanyiwa marekebisho.

“Nilimweleza Msajili kuwa katiba ya Chadema, inataka mapendekezo ya katiba yapelekwe kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, siku 30 kabla ya mkutano huo,  ukizingatia kikao cha Mkutano Mkuu kilifanyika Agosti 13, 2006 na kufanya mabadiliko ya Katiba  Julai 13, mwaka huo huo ndiyo iliandikwa barua, sasa hata kama barua ingesafirishwa kwa ndege ama kwa usafiri wowote lazima zingeanza kupokelewa kuanzia Julai 14 mpaka 16, hapo tayari siku zimepungua, si 30 tena,” alisema Mwigamba.

Alisema kuwa waraka huo uliosambazwa kwa wajumbe ulitakiwa kuwafikia siku 30 kabla na kwamba haukueleza iwapo mapendekezo hayo yaliandaliwa na Baraza Kuu ambalo linatoa mapendekezo kwa Mkutano Mkuu au la!

Alisema waraka huo, ambao alibahatika kuuona, ulikuwa hauna uzito unaostaili, kwani ulikuwa sawa na barua ya uchumba ambayo ni tofauti na cheti cha ndoa unachoweza kupeleka ushahidi Mahakamani.

Anasema wakati barua ya Akwilombe ikisambazwa ilikuwa pamoja na rasimu, ambapo yeye (Mwigamba) akiwa mmoja wa Makatibu wa Wilaya hakuona nakala yake.

Gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ili kupata ufafanuzi, hata hivyo hakuweza kupatikana, kutokana na kuwa katika vikao, huku simu yake ya kiganjani ikiwa haipatikani.

Alipotafutwa Msemaji wa Chadema, Tumaini Mkene, alishindwa kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa,  ambapo alisema suala hilo lilishazungumzwa katika mkutano wa waandishi wa habari na majibu yake yanajitosheleza

>>Mtanzania

WAZIRI WA FEDHA AKIRI SERIKALI KUWA KATIKA HALI NGUMU KIFEDHA




Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amekiri Serikali kuwa katika hali ngumu, lakini akasema kuwa mkakati uliopo ni kudhibiti matumizi ili yaendane na fedha iliyopo. 
 
Waziri Saada alisema hayo kwa njia ya simu, alipotakiwa na Mwananchi  kujibu madai ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) juu ya kauli yake ya hivi karibuni aliyoitoa katika mkutano mjini Dodoma.
 
“Ni kweli nimesikia alichosema CAG na nadhani alimaanisha kudhibiti matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji. Siyo kwa Tanzania tu, nchi zote huwa zinazingatia matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji yaliyopo” alisema Saada na kuongeza:
 
“Sisi kama wizara tumejipanga kukusanya na kutegemea fedha zetu za ndani kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA). Tunategemea misaada, lakini huwa inachelewa. Hata wakaguzi nao wanapaswa kuangalia hilo.”
 
Hata hivyo, Saada alisema kuwa Serikali ina fedha za kutosha kuendesha shughuli zake.
 
Alhamisi wiki hii CAG,Ludovick Utoh akifungua Mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ukaguzi nchini mjini Dodoma alisema, Serikali ya Tanzania iko hoi kifedha hivyo Bunge na Serikali lazima wajitathimini na kuongeza wanayo matumaini kutokana na ushauri ambao umekuwa ukitolewa na ofisi yake kufanyiwa kazi.

>>Mwananchi

SERIKALI YA TANZANIA YAIOMBA UINGEREZA MSAADA WA MABEHEWA NA INJINI ZA TRENI AMBAZO HAIZITUMII LAKINI NI NZIMA.




SERIKALI ya Uingereza inatafakari ombi la Tanzania la mabehewa na injini za treni, ambayo nchi hiyo haizitumii tena, lakini bado ni nzima kwa ajili ya kusaidia kuimarisha usafiri wa reli katika Tanzania na hasa wa Jiji la Dar es Salaam.

Ahadi hiyo ya Uingereza ilitolewa na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, Nick Clegg wakati wa mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete kwenye hoteli ya Sheraton, Davos, Uswisi, ambako viongozi hao wawili walikuwa wanahudhuria Mkutano wa Taasisi ya Uchumi Duniani (WEF) mwaka huu.

Katika mazungumzo yao katikati ya wiki hii, Rais Kikwete alizungumzia hatua za Serikali ya Tanzania za kuimarisha
usafiri hasa ule wa reli mjini Dar es Salaam na ile ya kwenda Bara.

Katika mazungumzo hayo ambayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Rais alimwomba Clegg kuangalia uwezekano wa nchi hiyo kutoa mabehewa na injini ambazo hazitumiki tena Uingereza ambako Rais alisema kuwa bila shaka bado zinafaa kwa Tanzania.

Akielezea hali ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli nchini, Waziri Mwakyembe alisema kutokana na uchakavu wa reli na ukosefu wa injini na mabehewa ya kutosha ni kiasi cha tani 300,000 tu za mizigo zinazosafirishwa kwa reli kati ya mizigo tani milioni 13.7 ambayo inasafirishwa nchini kila mwaka.

Alisema kuwa kiasi kilichobakia kinasafirishwa kwa barabara. “Mheshimiwa unaweza uzito wa ninayoyasema kwa sababu tunajenga barabara nyingi nchini, kila kona, lakini usafirishaji wa namna hii wa mizigo kwa barabara utaharibu kabisa barabara hizo katika muda mfupi,” Rais Kikwete alimwambia Clegg.

Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete aliishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya Tanzania kwa kusaidia nyanja za elimu, afya na maji na pia kuendelea kuwa nchi inayoongoza duniani kwa makampuni yake kuwekeza katika uchumi wa Tanzania. Rais pia alimwomba Clegg kusaidia kuvutia uwekezaji zaidi kutoka Uingereza kuja Tanzania kwa kuisemea vizuri Tanzania.

“Neno lako moja la kusifia Tanzania lina nguvu zaidi kuliko hotuba zangu kwa makampuni na wenye makampuni katika Uingereza.” Viongozi hao pia walizungumzia umuhimu wa kukamilisha Mikataba ya Ushirikiano wa Uchumi ya EPA kati ya nchi za Afrika na nchi za Ulaya.

Walikubaliana kuwa mjadala wa jambo hilo umechukua muda mrefu kupita kiasi na sasa ni wakati wa kufikia mwisho wa jambo hilo. Rais Kikwete alimwambia Naibu Waziri Mkuu huyo kuwa moja ya masharti ambalo yanayoikwaza Afrika katika kufikia makubaliano ya mikataba hiyo ni lile la kuzilazimisha nchi za Afrika kufungua masoko yao kwa namna ile ile ya yatakavyofunguliwa masoko ya nchi za Ulaya.

“Hofu yetu hasa ni kuhusu jambo hilo. Ni vigumu, kwa mfano, kwa makampuni ya ujenzi ya Tanzania kushindania tenda moja na kwa masharti yale yale na makampuni ya Uingereza kwa sababu wakati mwingine unaweza kufungua uwanja ukawa sawa lakini wachezaji wasiwe na uwezo unaofanana.”

Wakati wa mazungumzo hayo, Rais Kikwete alimkaribisha Clegg kutembelea Tanzania, ombi ambalo Naibu Waziri Mkuu alilikubali kimsingi akisema kuwa anatamani sana kuja tena Tanzania kwa sababu miaka 13 iliyopita aliitembelea Tanzania kwa mapumziko na mkewe baada ya kuwa wamefunga ndoa. -- via HabariLeo

Saturday, 25 January 2014

KOMPUTA ZA MAC ZATIMIZA MIAKA 30 TANGU ZIZINDULIWE

 Waanzilishi wenza wa Apple, Steve Jobs na John Sculley wakioneshwa kwa mara ya kwanza komputa Macintosh kwenye mkutano wa wawekezaji huko Cupertino, January 1984
Miaka 30 iliyopita Ijumaa hii takriban saa 3 na dakika 45 asubuhi, Jumanne, January 24, 1984, komputa za Macintosh zilizinduliwa na Steve Jobs mbele ya wawekezaji wa kampuni ya Apple kwenye mkutano wao.
“Hello. Naitwa Macintosh. Ni hakika ni vizuri kutoka nje ya begi hili,” kibox chenye uzito wa kilo nane kilisema kupitia sauti yake ya kiroboti.
Tangazo la Mac lilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye Super Bowl XVIII mwaka 1984, ambalo lilitajwa kuwa tangazo la TV bora zaidi kuwahi kufanywa

 

Miaka 30 baadaye kumeshuhudiwa maendeleo makubwa kwenye historia ya Mac, komputa ambayo imebadilisha jinsi dunia inavyoiona teknolojia leo.

Mwaka 1998, Apple ilizindua iMac, kwenye picha
Steve Jobs alikuwa CEO wa zamani na mwanzilishi mwenza wa Apple. Alifariki kwa ugonjwa wa saratani October 5, 2011.

MKUTANO WA DR SLAA WATIKISA MBEYA


Mabango Mbeya
Baadhi ya wananchi wa mji wa Mbeya wakiwa wabeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima wa Chadema, uliofanyika kwenye Uwanja wa Lwanda Nzovwe mjini Mbeya jana. Silinde kuhutubia Mbeya
Mbunge wa Mbozi Mashariki, Davi Silinde (Chadema), akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe mjini Mbeya jana.
Slaa kuhutubia Mbeya 1
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana. 





Slaa kuondoka Makongorosi
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, wakiondoka kwa shamrashamra, baada ya kuhutubia mkutano wa hadahara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Slaa na mtoto
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwa amembeba mtoto Sheila Shukurani (3), kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara matika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Sugu kuhutubia Mbeya
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya na vitongiji vyake katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana.
Picha na CHADEMA