Michuano
ya kombe la FA imeingia raundi ya tano ambapo mechi zote zitachezwa
Jumamosi na Jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi pili huku Chelsea na
Manchester City zikitazamiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Chelsea
walifuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo
ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila. Kocha wa Chelsea
Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii alisema: Iwapo unataka
kuwa bora lazima ucheze na timu bora.”
Pia Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2
Liverpool
wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano,huku
Roberto Martinez akiiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya
Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi
iliyokutanisha timu zote za ligi ya England.
Cardiff
watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton.
Sheffield watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship,
Charlton FC.
Mshindi
wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na mshindi kati
ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe
hilo ambalo fainali yake itachezwa kwenye uwanja wa Wembley.
Source:BBC
Source:BBC
0 comments:
Post a Comment