Kuzima smartphone saa 3 usiku kunaweza kukufanya ufanye kazi vizuri siku inayofuata, watafiti wamesema
Tunafahamu usiku unaweza kuwa muda mzuri wa kupitia status za washkaji
Facebook, kutazama picha mbalimbali Instagram ama kufuatilia mijadala
kwenye Twitter lakini hicho kinaweza kuwa kikwazo kikubwa cha nia yako
ya kutaka kupata usingizi wa kutosha ama kuwa na utendaji mzuri kazini.

Watafiti hao wanasema kujiondoa kabisa na matumizi ya simu usiku ni njia ya kupata usingizi mzuri usiku. Wamewaomba waajiri kusubiri kutuma email hadi asubuhi
Timu
katika chuo kikuu cha Washington imesema matumizi ya simu usiku sana
yanaweza kuharibu kabisa usingizi wako na namna utakavyofanya kazi siku
inayofuata. Wameshauri wafanyakazi wawe na tabia ya kuzima simu ama
lasivyo watajikuta wakishindwa kufurahia kazi kesho yake.
“Sababu
ya hii kama tutakavyoelezea, ni kwamba smartphones ni mbaya kwa
usingizi, na usingizi ni muhimu kwa uchapakazi wa mwajiriwa,” alisema
Christopher Barnes, Profesa Msaidizi katika chuo kikuu cha Washington
(Foster School of Business) aliyeongoza utafiti huo utakaochapishwa
kwenye jarida la , Organizational Behavior and Human Decision Processes
baadaye mwaka huu.
“Bahati
mbaya smartphones zimetengenezwa mahsusi kuharibu usingizi. Sababu
zinatufanya kiakili kuendelea na kazi hadi usiku, zinafanya kuwepo ugumu
wa kujiondoa kisaikolojia kutoka kwenye masuala muhimu ya siku ili
tupumzike na kulala. Pengine suala gumu kuliepuka kutoka kwenye
smartphones ni kwamba zinatuweka kwenye mwanga, ukiwemo mwanga wa blue.
Hata kiwango kidogo cha mwanga wa blue hupunguza uzalishaji wa kemikali
ya usingizi, melatonin, ikimaanisha kuwa muonekano (display) unaweza
kutengeneza madhara haya.
0 comments:
Post a Comment