Monday, 27 January 2014

JE UNAJUA KUWA MTO MSIMBAZI, UKITUMIKA VEMA UTAWEZA KUPUNGUZA FOLENI JIJINI DAR ES SALAAM?


Mto Msimbazi ni mto mkubwa sana ambao unaweza kutumika kwa usafiri, moja ya kupunguza adha ya foleni barabarani ni kuutumia mto msimbazi kwa usafiri.

kuanzia Salender Bridge, Muhimbili, Jangwani hadi Vingunguti, na sehemu nyingine ulipopita.  Wale watengenezaji plan za miji wangeweza kufikiria jinsi ya kuufanya mto huu kuwa kivutia hapa Mkoani Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wataalamu wengine.

Kila ninapo kaa na kuuangalia mto huu naona kuna kiasi kikubwa sana cha fedha mkoa kama mkoa na wananchi wake tunakosa, pia ni sehemu nzuri sana kwa kufanyia sehemu za burudani na mandhari nzuri zitakazo weza kuwavutia wawekezaji wa ndani zaidi na nje kuweza kufanya biashara katika maeneo yaliyopita kwa kuweka Hoteli, Migahawa, Nyumba za Kulala wageni, Sehemu za sherehe, Boti za kusafirishia abiria, mandhari nzuri za bustani.
Mimi sio mbunifu wa kuchora, wa kupamba lakini najua wapo wataalamu wanaoweza kutengeza ramani, picha, na jinsi ya kuyatengeneza maji yaweze kuwepo muda wote kwa kiwango kinachotakiwa ili boti ziweze kupita kwa miaka yote bila kuathirika na upungufu wa maji au takataka.  Nikiwa kama mtanzania ninayependa maendeleo ninaiona Tanzania tofauti kidogo na wenzangu kuna vitu vingi tunaweza kuvifanya katika mto huu wa Msimbazi na tukaweza kupata kipato kwa uvuvi, usafiri na mambo mengine mengi yatayobuniwa na kuwekwa pale, pia ni ajira kwa vijana, hapa ndipo pa kupatia ajira vijana wengi.





Nadhani wazo hili litakuwa na mantiki zaidi kama wataalamu wa Wizara husika na wananchi watatumia busara, hekima na utashi walio nao na kugombea mambo yasiyo na tija, tunaweza kwa silimia mia kuutumia mto huu kwa tija, na tusifikirie bonde la mto msimbazi tu kama bonde, tufikirie mto kama mto, maana sasa hivi mto ule hauonekani kwa kuwa umefunikwa na ujenzi wa vijijumba, majumba na kilimo, pia na kuwa sehemu kubwa ya utupaji taka.  Sidhani kama kazi hizi ndizo zinazotakiwa kufanyika katika mto huu.
Kuna wateja wengi sana ambao wanaweza kuutumia mto huu kuanzia mjini hadi vingunguti, kuna mabilioni ya shilingi tunaweza kuyapata kupitia mto huu, ni kiasi cha kubuni cha kufanya tu chenye tija.  Nimetoa mada moja inayosema jinsi ya kuyafuga maji tunaweza kuyafuga kwa kuyaingiza maji ya mvua katika mto huu kwa faida na kuweza kuutumia na kuingiza kipato kwa mkoa mzima.
Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Madiwani, Mameya na Waziri wa Wizara zinazohusika mnaweza kukaa na wataalamu mkapanga la kufanya ili itokee mwisho wa siku kuwe na njia ya usafishaji wa kupitia mto Msimbazi, na msiwaze tu labda kuwe na uwazi wa kutengeneza sehemu ya michezo, tuutumie mto huu kwa tija.  Tusilifanye jambo hili kisiasa, tusiogope wananchi kulalamika kwa sasa, ila mwisho wa siku wataelewa namaanisha nini.  Watanzania tunatakiwa kuwa wabunifu na kuufanyia kazi ubunifu huu kwa manufaa ya nchi na wananchi na mwisho wa siku tufaidi wote.


Wana blog tutoe mawazo kwa michoro na picha ili tuijenge nchi yetu. 

Inawezekana kabisa Mto huu ukiboreshwa ukawa na faida kama baadhi ya mito hii hapa.








BUBERWA ROBERT BLOG

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment