Picha
wa tatu kulia,ni Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara
Promotions,Bwa.Simai Mohamed akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani)
mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun,jijini dar kuhusiana na
ujio wa tamasha la muziki la Sauti za Busara la 11 katika
kusherehekea utamaduni na muziki wa Afrika.Bwa.Simai amefafanua kuwa
mwaka huu tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 13 mpaka februari 16
katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
Pichani
ni Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo,aitwaye
Jhiko Man pichani akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo
chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo
asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Mmoja
wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara,aitwaye
Ashimba pichani nae akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo
chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo
asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Kwa Tarifa mbalimbali za tamasha hilo tembelea www.busaramusic.org.
Jumla
ya Vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100 live.Bwa
Simai amesema kuwa vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi
ya 560 na vinawakilisha nchi 19,ameongeza kuwa zaidi ya wasanii 200
watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki,wasanii hao wanatoka
Afrika Mashariki,Afrika Kusini na Magharibi,maeneo ya mto Nile na pia
kutoka Puerto Rico.
Kutoka
Tanzania,Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni
Jhikoman,Ashimba,Swahili Vibes,Hoko Roro,Seven Survivor,Abantu
Mandingo,Segere Original na Kazimoto.
0 comments:
Post a Comment