Waandamanaji wakipambana na polisi mjini Kiev
Vifo
hivyo ni vya kwanza tangu kuzuka kwa maandamano ya kuipinga serikali
miezi miwili iliyopita. Waandamanaji na polisi nchini Ukraine
wamepambana tena mapema leo (23.01.2014), baada ya ghasia kuzuka hapo
jana Jumatano na kuigeuza sehemu ya katikati ya mji mkuu, Kiev kuwa
uwanja wa vita, huku polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi
za mpira dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.
Vifo
hivyo vimezusha hofu mpya baada ya miezi miwili ya maandamano ya
kuipinga serikali yaliyochochewa na hatua ya serikali kutosaini
makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na Umoja wa Ulaya, kutokana na
shinikizo la Urusi.
Moshi
mweusi ulifuka kutokana na magurudumu kuteketezwa wakati wa vurugu hizo
mjini Kiev, huku picha za magari ya kivita yakitumiwa kupambana na
waandamanaji hao.
Makabiliano
hayo yanakuja baada ya siku moja ya kubuniwa sheria mpya za kuharamisha
maandamano wiki jana. Bunge liliidhinisha sheria hizo wiki jana na
kusababisha vurugu mpya
Viongozi
wa mashitaka walithibitisha kuwa watu wawili walifariki kutokana na
majeraha ya risasi. Ni watu wa kwanza kufariki kutokana na vurugu tangu
kuanza Novemba mwaka jana kutokana na mapendekezo ya serikali kujiunga
na muungano wa Ulaya
Waandamanaji
walianza, kuwatupia mabomu ya petroli na mawe wakati polisi wa
kupambana na ghasia nao waliwatupia magurunedi na risasi za mipira
0 comments:
Post a Comment