Mpenzi
wa siku nyingi wa mmiliki wa club ya Chelsea na bilionea wa Urusi,
Roman Abramovich aitwaye Dasha Zhukova,ameomba radhi kwa picha yake
inayomuonesha akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa umbo la
mwanamke mweusi aliye nusu mtupu.
Picha
hiyo iliyokuwa imewekwa kwenye interview aliyofanyiwa na mtandao wa
masuala ya mitindo wa Buro247.ru, ilisambaa Jumatatu hii wakati ambapo
Wamarekani walikuwa wakisherehekea siku ya Martin Luther King Jr. Day
aliyekuwa mtetezi wa watu wamarekani wenye asili ya Afrika.
Picha
hiyo ilipunguzwa na kumuonesha Zhukova na sehemu tu ya kiti hicho baada
ya kuleta mjadala mkubwa mtandaoni kutokana na kuwa kibaguzi.Kwenye
maelezo yake yaliyochapishwa na gazeti la The Moscow Times, Zhukova
alisema kutumika kwa picha hiyo ni kitendo cha kujuta hasa katika siku
ya Martin Luther King Jr na kwamba yeye si mbaguzi wa rangi.
Sehemu ya maelezo yake inasomeka: This
photograph, which has been published completely out of context, is of
an art work intended specifically as a commentary on gender and racial
politics. I utterly abhor racism, and would like to apologize to anyone
who has been offended by this image
Wanaharakati mbalimbali wamemtuhumu Zhukova kuwa anapigia debe utumwa.
0 comments:
Post a Comment